>>>Naam mjumbe umekua ukiskia stor tofauti zikizungumzia juu ya Dark web lakini je umewai kujiuliza au kufanya utafiti ukajua kiundani zaidi maana halisi na ukweli wote kuhusu Dark web?Basi Leo nakuletea mambo yote unayopaswa kuyajua kuhusu hii dark web
>>>kwa kuanza tuangalie nini maana ya dark web kama ifuatavyo:
NINI MAANA YA DARK WEB??!!
>>>Ni mkusanyiko wa tovuti(website> ambazo hazipatikani kwenye search engine za kawaida (google,bing,Safari na Yahoo)
>>>Kabla hatuzama kiundani zaidi Dark web ni kinyume cha surface web au clean web.Surface web ni internet tunayotumia sisi mfano kuperuzi,Youtube,whatsApp n.k lakini dark web ni tovuti ambazo sio rahisi kufikika kama zilivyo surface web ambazo ndio wengi tunatumia
>>>Ukizungumzia Dark web basi utakua unaongelea Internet na Internet imegawanyika katika vipengele saba ambapo kipengele cha juu ni Surface web ambacho ndio wemgi tupo apo lakini ni kipande kidogo sanaa katika INTERNET.
>>>Kama unavyoona pichani wataalamu wanapenda kutumia mfano wa mlima wa barafu(Iceberg) kuielezea dark web.Sehemu ya juu ndio Surface web ambayo ndio nafasi ndogo sana katika internet lakini ndio 90% ya watu wanaitumia. Na sehemu iliobaki haonekani kwa sababu iko chini lakini ndio kubwa zaidi kwenye utawala wa Internet na ni ngumu kufikika iyo ndo inaitwa Dark web
>>>Pia unapoingia Dark web unakua sehemu nyeti na unakua haujulikani(Anonymous)Kwasababu Dark web inaficha IP ADDRESS Ambayo ndio Utambulisho wa mtu mtandaoni.Hivyo basi ukiwa katika Surface web pia utakua unafatiliwa na usalama wa mtandaoni wa nchi husika uliyopo endapo ukienda kinyume na sheria za nchi basi usalama wa mtandaoni watakutia mkononi hii yote ni kwa sababu ya IP ADDRESS yako inayoonesha sehemu uliopo na ndio sura/utambulisho/identity yako ya Mtandaoni
>>>Unyeti na usiri wa Dark web ndio umepelekea ionekane ni sehemu ya uhalifu pekee lakini sio kweli Dark web ni mahali unapoweza kufaidika napo endapo utatumia vizuri kwa mujibu wa sheria za nchi yako.
>>>Ukiwa katika Surface web ambayo ndio tupo wengi mfano ukiingia Google ukasearch kitu basi google wataangalia Ip adress yako itawaonesha mahala ulipo(TRACKING)na kukuletea vitu sahihi unavyovitafuta,Haiishi apo pia itajua wewe ni mtu wa aina gani kama unasearch sana Ngono watajua wewe ni kijana pia watatumia data izo kukufikishia matangazo ukitaka kuamini search kitu mara mbili google alafu urudi Facebook utaona page zinazousiana na ile mada ulioitafuta google hii yote ni kwasababu wanajua taarifa zako na unachokifanya wanakiona lakini unapotumia Dark web hakuna mtu wakukujua wala kukufatila unapokuwa mtandaoni.
TOFAUTI YA DARK WEB,DEEP WEB NA DARK INTERNET.
>>>Unapozungumzia Dark web lazima utakutana na hii misamiati inayotaka kufanana lakini pia imetofautiana katika utendaji wake wa kazi.
Deep web:Huu ni mkusanyiko wa Kurasa ambazo haziifadhi data za mtumiaji na hazipatikani Surface web au clean web mfano uwezi kuzipata google,yahoo,safari,bing n.k
>>>Yaani ni mkusanyiko wa website ambazo hazipatikani Clean web kama vile huwezi kuzipata Google,Safari,Yahoo au search engine yoyote ile ya Surface web.kwaio deep web ni tovuti nyeti zaidi kuliko zote katika Internet.
Dark web:Huu ni mkusanyiko wa tovuti website ambazo hazipatikani au haziwezi kufikiwa na Search engine za Surface web/clean web kama google lakini ukiwa na Search engine maalum unaweza kuzifikia tofauti na deep web ambazo ziko chini zaidi na ngumu sana kuzifikia ata mtu akupe link zake
>>>Hizi ni tofauti na deep web ambapo ndani ya deep web tovuti za deep web ni ngumu ku share na kufikika lakini Dark web ni myeti lakini unaweza kushare link na mtu akaingia kwenye iyo tovuti.
Dark Internet:Unaweza kfikiri Dark web na Dark internet ni kitu kimoja lakini hapana Dark internet ni Data maalum zinazotunzwa katika mtandao wa Dark web kwa lengo la kuwa siri.kwa mfano wanasayansi wanatumia Dark Internet kutunza Taarifa zao za utafiti ili kuzuia kufatiliwa na kuvuja katika Surface web.kwaio wanaziweka taarifa kuwa siri
NI YAPI MATUMIZI YA DARK WEB??!!...
>>> Kutokana na Sifa ya Unyeti na Usiri wa mtumiaji uliopo Dark web kuna stori nyingi zinasema kuwa Dark web ni sehemu ya Uhalifu lakini Si kweli Dark web haikuanzishwa kwa Lengo la uhalifu bali Sifa yake ya kumfanya mtu Asijulikane ni nani na yuko wapi ndio imesababisha ongezeko la uhalifu ndani ya Dark web tuangalie baadhi ya uhalifu unaofanyika uko Dark wek kama ifuatavyo:
1.BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA.
>>>Kama ulikua ujui ni wapi madawa ya kulevya yanaponunuliwa basi ni Dark web kwenye soko linaloitwa THE DARKNET MARKET Ni kupitia Dark web ndio mahali wauzaji na wanunuaji wengi wa madawa wanapowasiliana na kufanya biashara hii ni kwasababu Dark web haiifadhi data za mtu husika kama ilivyo kwenye Tovuti za Surface web kama google n.k Hii imewafanya wafanyabiashara wengi wajihisi wako sehemu salama
>>>Hata ivyo FBI hawako nyuma kuchunguza wamiliki wanaoendesha Tovuti mbali mbali za madawa na kuwakamata lakini wakikamata mmoja wanaibuka wauzaji wapya wengi zaidi kuna tukio liliitwa THE SILK ROAD hili ni Soko lliokuwa la watukutu na magwiji wa madawa mwisho wa siku walitiwa nguvuni lakini yalizuka makundi mengine mengi
2.UUZAJI WA VITU HARAM(MAGENDO)
>>>Sio madawa tu lakini kama unaskia watu wanauza viungo vya binadamu kama Figo basi biashara hizo zinafanyika kwa asilimia kubwa dark web.Pia uuzaji wa kadi za benk zilizodukuliwa pia kunauuzaji wa nyaraka muhimu za makampuni au Serikali za nchi mbali mbali.
3.UUZAJI WA SILAHA
>>>Umekuwa ukiskia watu wanakamatwa kwa kumiliki silaha kinyume na Sheria lakini unajiuliza awa watu wanatolea wapi izo silaha basi Tambua kuwa Dark web ndio mahala ambapo kuna uuzaji na ununuaji wa Silaha kinyume na sheria silaha kama bunduki mabomu na nyingine nyingi zinapatikana Dark web.
4.PICHA ZA UNAJISI WA WATOTO(Child ponography)
>>>Pia Dark web kuna tovuti zinazosambaza picha na video zinazoonesha unajisi wa watoto jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili ya Nchi nyingi
5.NJIA NZURI YA MAWASILIANO.
>>>Kuna tovuti za nchi kadha wa kadha ambazo huwezi kuzifikia kwa sababu zimetengenezewa mfano wa ukuta (Firewall) ambapo IP ADRESS yako ikiwa tofauti na Nchi iyo huwezi kuiingia na kuperizi Tovuti hiyo lakini kupitia Dark web utaweza kuingia tovuti yoyote ile
>>>Pia mwaka 2005 China ilipiga marufuku matumizi ya VPN(Virtual Private Network) Ni sofware zinazokupa ulimzi kwa kuficha IP Address yako ukiwa mtandaoni ivyo ilipelekea wachina wengi kutumia dark web kama Njia ya mawasiliano ili kuepusha kufatiliwa(Tracking)
6.PROFESSIONAL HACKERS(Wadukuzi waliobobea)
>>>Pia ukizingumzia wadukuzi/hacker basi Dark web ndio makazi au makutano yao na kazi zao zinapofanyikia,Sifa za Dark web zinafanana sana na sifa za wadukuzi kwani wadukuzi hawapendi kufatiliwa(tracked)
>>>Ndani ya Dark web utakutatana na makundi makubwa yanayoweza kukufanyia kazi yoyote inayohusu udukuzi wa mitandaoni pia kuna baadhi ya website/tovuti utakuta hacker wanauza kadi za benki zilizodukuliwa pia utakuta Leseni feki za gari pia wanauwezo wa kukutengenezea ID feki ya Nchi husika pia wanadukua kadi zinazofanya manunuzi mtandaoni kwenye makampuni kama Amazon,Ebuy,Alie express na ata kikuu na kuziuza njia hii inaitwa carding.
7.DARK WEB NJIA SALAMA YA WAVUJISHA SIRI ZA SERIKALI(Whistleblowers)
>>>Pia Dark web inatumiwa sana sana na waandishi wa habari ili kutoa siri mbalimbali za mambo yanayoendelea katika nchi mfano kutoa picha,video na sauti za viongozi wanaopanga kuuhujumu/kula rushwa.Kwakua Dark web haitunzi data za mtumiaji ivyo ni rahisi kutoa siri bila wasiwasi wowote
NB:Dark web sio uhalifu na haipingani na Sheria zozote za nchi lakini unapoitumia kwa kufanya uhalifu apo ndo utakuwa kinyume na Sheria.
JINSI YA KUINGIA DARK WEB.
>>>Sasa umeshaijua Dark web kiasi flani na unashauku ya kuingia katika mtandao huo lakini kuingia huko usifikiri ni ngumu saaana hapana ni rahisi sana kuingia Dark web kwenye kifaa chako(Simu,Tablet au Kompyuter)
Hatua za kufata ni kama ifuatavyo.
1.DOWNLOAD TOR BROWSER
>>>Kitu cha kwanza inabidi upakue TOR browser. TOR browser ndio itakayokuwezesha kuifikia Dark web kwa sababu haitunzi data zako ivyo inakufanya usijulikane wewe ni nani na unatokea wapi kama zilivyo sifa za TOVUTI za Dark web Bonyeza hapa kudownload TOR BROWSER
>>>Ukishakua na TOR BROWSER utaweza kutembelea hata website za Surface web kama za google tofauti ni kwamba ukiwa Surface web kama google utakua unafatiliwa unajulikana mahali ulipo lakini ukitumia Tor browser Utambulisho wa wako unakua wasiri unaweza kuwa Tanzania lakini Serve zikakuonesha Upo Canada hii ndio maana ya Private explore
LINK ZA DARK WEB.
>>>Ili uifikie dark web sasa inabidi ujue link za tovuti unazotaka kuzitembelea na Link za Dark web zinabadilika kila mara na zinajumuisha mkusanyiko wa herufi na namba pia zinaishia na neno .onion tofauti na link za Surface web zinazoishiwa na .com Tazama mfano wa link kwenye picha
>>>Pia Dark web ni sehemu unayoweza kufurahia kwa kucheza game mbalimbali pia unaweza kutumia Dark web kuelimika kuhabarika na kuburudika ukitaka link zaidi za dark web bonyeza hapa
KWANINI DARK WEB INAONEKANA NI MAALUM KWA UHALIFU
>>>Sababu kuu ni uwepo wa BITCOIN na sarafu nyingine za mtandaoni
>>>Matumizi ya sarafu izi za BITCOIN yanamuwezesha mtu kulipa na kupokea pesa bila uhitaji wa benki na data au taarifa nyingine binafsi ni tofauti na zamani ambapo ukitaka kumtumia mtu wa nje pesa ni lazima utatumia Benk lakini kwa mfumo huu wa Cryptocurrency unafanya mtumiaji na mpokeaji watumiane pesa wao kwa wao na ni haraka na salama zaidi
>>>Hivyo uwepo wa bitcoin umepelekea ongezeko KUBWA SANA la uhalifu wa mtandaoni kama Udukuzi na mengine mengi.
>>>Hivyo haya ni mambo machache ambayo inabidi uyafahamu kuhusu mtandao huu wa DARK WEB
Usisahau kujoin Channel ya Telegram kwa habari nzuri zaidi BONYEZA HAPA
Pia unaweza kuchangia maoni yako au maswali katika kibox cha maoni(Comment) Apo chini
Usisahau ku-subscribe kwa email yako pia like,comment na share zaidi
MWISHO
❤❤❤❤❤❤❤❤❤
Comments
Post a Comment
nini maoni yako